Samaki mkunje angali mbichi
Udongo ufinye ungali maji
Kijana mfunze angali mchanga
Mweleze ajue hapa ni Misri
Si tena faraja sasa ni dhiki
Si ufalme kamwe sasa ni utumwa
Ondoka kutoka kwa Firauni
Chunga usipotee pale jangwani
Jenga uwezo wa kumalizia
Kukombolewa pekee hakutoshelezi
Haitoshi kujua waenda Kanaani
Kukomaa kiroho ndio la maana